Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage amesema kuwa anachohitaji ni kuwepo na viwanda endelevu ambavyo vitatoa ajira ya kutosha kwa watanzania.

Mwijage amesema kwamba baada ya kufanikiwa kuwafahamisha watanzania kuhusu viwanda na nchi nzima kuanza kuzungumzia viwanda sasa changamoto imekuja ya kukidhi viwanda kwa nchi nzima vyenye kuweza kuwa sifa zinazohitajika

Amesema kuwa “Unajua shida yangu siyo viwanda. Lakini ninashida na viwanda endelevu ambavyo vitawakidhi watanzania wote.  Vitengeneze ajira pamoja na bidhaa mbali mbali na zenye ubora kwenye jamii inayowazunguka, hicho ndicho kiwanda mimi ninachokitaka,”.

Waziri Mwijage amesema anapata changamoto kwa sasa baada ya kufanikisha uelewa kwa wananchi kuhusu viwanda sasa mahitaji ya viwanda yamekuwa makubwa kiasi kinachomfanya kushindwa kukidhi mahitaji ya watanzania wote.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *