Klabu wa West Bromwich wamemfukuza kocha wake, Tony Pulis baada ya matokeo mabovu wanayoyapata kwenye mechi za ligi kuu nchini Uingereza.
West Brom wapo kwenye mstari wa kushuka daraja baada ya kutopata ushindi hata mmoja katika mechi zake 10 ilizocheza.
Albion waliwezahinda mechi zake tatu za kwanza msimu huu lakini wameweza kutoka sare mechi nne na kupoteza saba tangu ilipoishinda Accrington katika kombe la Carabao 22 mwezi Agosti.
Aliyekuwa mkufunzi wa zamani wa klabu hiyo Gary Megson ambaye alikuwa naibu wa Pulis anachukua mahala pake hadi timu hiyo itakapotoa tangazo jingine.
Mwenyekiti wa klabu hiyo John Williams aliongezea:Uamuzi kama huu hauchukuliwa kwa urahisi lakini kwa sababu ya maslahi ya klabu.
Tuko katika biashara ya kupatamatokeo mazuri lkini kutokana na matokeo mabaya ambayo yamekuwa yakishuhdiwa kufikia mwishoni mwa msimu uliopita na kufikia sasa matokeo yamekuwa mabaya.
West Brom inakutana na Tottenham ika ligi ya Uingereza katika uwanja wa Wembley siku ya Jumamosi.