Mwanamitindo wa Bongo, Hamisa Mobetto amekanusha kukutana na Diamond Platinumz nchini Dubai wiki iliyopita ambapo Diamond alikwenda kwa ajili ya tamasha la One Africa Music.
Hamisa Mobeto amefunguka hayo baada ya kuenea taarifa kuwa mwanamitindo ameonekana na Diamond nchini Dubai jambo ambalo mwanadada huyo amelipinga vikali.
Habari hizo zilidai kuwa Diamond na Hamisa wameonekana pamoja nchini Dubai ambapo Diamond alikuwa anashiriki kwenye tamasha la One Africa Music Festival.
Picha mbali mbali zilisambaa mtandaoni zilizoashiria kuwa Diamond na Hamisa walikuwa katika eneo moja huku watu wakidai kuwa wamewaona pamoja kitendo ambacho kiliibua maswali Mengi kutokana na kuwa kiukweli Diamond yupo katika uhusiano na mama watoto wake na mpenzi wake Zari ambaye kwa sasa yupo nchini South Africa.
Pia Hamisa alifunguka na kudai kuwa yeye hana ugomvi wowote na familia ya Diamond hasa mama yake na Diamond kwani anamheshimu sana na pia anaamini mtu mzima hakosei lakini pia amedai anaelewa kama Zari anamchukia lakini yeye hana tatizo naye.