Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Zimbabwe cha Movement for Democratic Change (MDC), Morgan Tsvangirai amerejea nchini humo akitokea Afrika Kusini.
Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa chama hicho imesema kiongozi huyo aliwasili kimya kimya jijini Harare Jumatano ya wiki hii akitokea Afrika Kusini.
Tetesi kutoka kwenye vyombo vya Habari kutoka nchini Zimbabwe zinadai kurejea kwake kunazidisha uvumi wa kuafikiwa kwa makubaliano ya hali ya kisiasa baada ya Kuagushwa kwa Rais Robert Mugabe.
Kiongozi huyo wa upinzani amekuwa akipata matibabu ya saratani nchini Ureno na Chama chake tayari kimeeleza kuwa ndani ya masaa 24 Bw. Tsvangirai atazungumza na waandishi wa habari.