Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesogeza mbele kesi inayomkabili video Queen wa Bongo Agnes Masogange.

Mrembo huyo ambaye anatuhumiwa kwa kesi ya utumiaji wa madawa ya kulevya ambapo imeahirishwa kutokana na Mawakili wake kushindwa kumuandaa mapemba kwa ajili ya kujitetea.

Masogange anadaiwa kati ya Februari 7 na 14 mwaka huu katika maeneo yasiyojulikana katika jiji la Dar es Salaam alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin.

Kesi hiyo inatarajiwa kuendelea tena Mahakamani hapo January 17 mwakani baada ya kuhairishwa leo katika mahakama yanKisutu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *