Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Belle 9 amesema kuwa amesikitishwa na kifungo cha Lulu lakini yeye ameamua kukaa kimya juu ya suala ilo kwa sababu ameona watu wengi wamegeuza ushabiki.

Tangu kifungo cha miaka miwili cha muigizaji Lulu Michael kitangazwe siku ya Jumatatu mastaa mbalimbali wamekuwa na maoni tofauti na hata wengine kubishana baada ya kugawanyika huku wengine wakiwa upande wa Lulu huku wengine wakiegemea upande wa Kanumba.

Wasanii kama Mrisho Mpoto na Afande Sele wameingia katika majibizano makali mtandaoni baada ya kila mmoja kuegemea upande wake na kuamini anachotaka kuamini.

Belle 9 amesema kuwa kwake yeye imekuwa ngumu kuongea chochote juu ya kesi hiyo siku hizo zilizopita kwani anaamini kuwa kuna wasanii wanashabikia kesi hiyo kwa sababu zao binafsi:

Pia Belle 9 aliwasihi wasanii wasigeuze kifungo cha Lulu kama njia ya kufanyia bishara au upepo fulani wa trending ili tu waonekane mbele za watu kuwa bado wapo kwenye ramani.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *