Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema kuwa aliyekuwa mwanachama wao, Lawrence Masha hakuwa na msaada wowote ndani ya chama hicho.
Amesema kuwa kuondoka kwa Masha katika Chama hicho hakijatikisika chochote bali kinazidi kuimariki na kupokea wanachama wengi wapya, hivyo kuondoka kwa mtu asiyekuwa na msaada ndani ya chama hicho si tatizo.
Mbowe amesema kuwa Masha hajasaidia chochote ndani ya chama hicho kwasababu hajafanya chochote akiwa ndani ya Chadema.
Masha alitangaza uamuzi wa kuondoka Chadema kupitia taarifa yake iliyosambazwa kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ya kuamua kuachana na Chadema huku akisema chama hicho kinasafari ndefu ya kuweza kutwaa dola.