Video queen maarufu Bongo, Gigy Money amesema kuwa ni kweli sehemu ambayo anayoishi kwa sasa hapafanani na yale anayoyafanya lakini hajutii hilo.

Gigy Money amesema kuwa nyumba ambayo imeonekana anaishi sasa amehamia hivi karibuni baada ya nyumba aliyokuwa anaishi awali kujaa maji na kusomba vitu vyake, kutokana na mvua zilizoleta mafuriko hivi karibuni.

Gigy Money ameendelea kwa kusema kwamba kitendo cha mafuriko kusomba vitu vyake kimempa mawazo kwani imemlazimu kuanza moja kwenye maisha, pamoja na kutafuta nyumba yoyote ile ili aanze maisha upya.

Amesema kuwa hajutii maisha hanayoishi kwasasa kwasbabu siyo ni kawadia tu kukaa anapoishi sasa lakini maisha ndiyo yalivyo na yeye pia ni binadamu anaweza kuishi maisha yoyote.

Hivi karibuni kumeibuka minong’ono kwa baadhi ya watu wakionesha kushangazwa na kitendo cha Gigy Money kuishi kwenye nyumba ambayo haieleweki wakati mitandaoni anajitapa kuvaa vitu vya gharama kubwa zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *