Mshambuliaji wa Manchester United, Romelu Lukaku ameweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote katika timu ya taifa ya Ubelgiji.
Vijana hao wa Roberto Martinez waliifunga Japan bao 1-0 huko Brugge na Lukaku kuweka rekodi hiyo.
Lukaku alifunga goli la 31 kwa nchi yake pale alipomalizia krosi safi kutoka kwa Nacer Chadli aliyoiingiza wavuni kwa kutumia kichwa.
Lukaku alikuwa ametoshana na Bernard Voorhoof na Paul van Himst walipokuwa na magoli 30 kila mmoja wiki iliyopita.
Ubelgiji waliendeleza msururu wao wa kutoshindwa hadi mechi 15.
Mara yao ya mwisho kushindwa ilikuwa mikononi mwa Uhispania mechi ya kirafiki Septemba 2016.
Kwengineko, Uholanzi walipata ushindi wao wa pili tangu kukosa nafasi ya kushiriki katika Kombe la Dunia nchini Urusi walipopokeza Romania kichapo cha magoli 3-0 huko Bucharest.