Muigizaji wa Bongo Movie, Rose Ndauka amefunguka na kudai kuwa kifo cha Kanumba ni kikubwa kuliko hukumu ya kuua bila kukusudia aliyopewa muigizaji Lulu Michael.

Elizabeth Michael ‘Lulu’ amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela mapema wiki hii baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia mpenzi wake Steven Kanumba.

Rose Ndauka amesema kuwa Hili jambo lililotokea limenigusa kwa sababu najifunza mambo mengi najifunza kuwa kwenye maisha kuna kitu kinaweza kukukuta ambacho hujawahi kutarajia lakini vile vile kimenigusa kwa sababu pengo la Steven Kanumba halijaweza kufutika hasa kwenye mioyo ya Watanzania wengi, nikijiongelea mimi kama msanii lakini pia nikiongelea Watanzania waliokuwa wanapenda filamu za Steven Kanumba lakini pia kwa upande mwingine kimenigusa kwa sababu Lulu bado ni binti mdogo lakini mwisho wa siku Mungu ana mipango yake”.

Lakini pia Rose ameongelea kuhusu post yake aliyoiweka kwenye kurasa yake ya Instagram na waty wengi kutafsiri kuwa alikuwa upande Wa Kanumba:

Kwenye ile posti nilikuwa namaanisha kwamba vijana tujifunze kutokana na tukio zima  lililotokea kwa Kanumba na kusababisha kifo chake lakini vile vile kwa upande mwingine like tukio limemsababishia kifungo msanii Lulu Michael lakini piano lulu anatakiwa amuombe sana Mungu kwani hakuna linalomshinda kila kitu kinawezekana lakini pia atatumikia kifumgo kitapita lakini Kanumba ameenda moja kwa moja kwaiyo pia hiyo miaka miwili haiwezi kulipiza maisha ya Kanumba aliyopoteza muhimu ni kusameheana na kuendelea na maisha”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *