Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Barakah The Prince amesema kuwa hajawahi kugombana na msanii yeyote ila kusema kwake ukweli ndio kunafanya watu kumchukulia kama mkorofi.

Baraja amesema kuwa baada ya kuligundua hilo ameamua kulifanyia kazi baada ya kushtumiwa na mashabiki wake.

Amesema kuwa “Sijawahi kumtukana msanii au kugombana na msanii but ule ukweli wangu labda unamwambia mtu, unajua watu wengi hawapendi kuambiwa ukweli, anaweza akakuboa ukamwambia ukweli akakuchukulia tofauti kwa hiyo nadhani sana hiyo ndio ilikuwa inachangia”.

Ameongeza kwa kusema kuwa “Wakati huu nimejitahidi ndio maana hata nimekaa kimya muda mrefu sana, nimejaribu kukaa na watu wengi sana wamenipa cancelling wakiwemo watu wakubwa kwenye entertainment”.

Pia meongeza kuwa watu kwa sasa watamuona ni Barakah mpya kwani anajichukulia kama msanii mpya ambaye ndio anataka kutoka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *