Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amedai kwamba ameshtushwa sana na mapendekezo ya serikali kuhusu kuwekeza pesa kwenye miradi ambayo inaweza kuendeshwa kibiashara.
Nape amesema kwamba baadhi ya miradi ambayo ingeweza kutekelezwa na sekta binafsi ni ujenzi wa reli ya kisasa ya kati, mradi wa umeme Rufiji, mradi wa bandari na uboreshaji shirika la ndege.
Nape amesema kwamba aliposoma mapendekezo alishtuka baada ya kuona kwamba Serikali inapendekeza kuwekeza pesa za Serikali kwenye miradi ambayo inaweza kuendeshwa kibiashara ambayo pia watu binafsi wangeruhusiwa kuiendesha.
Akiendelea kusimamia hoja yake Nape amesema kuwa miradi hiyo ni mikubwa na itagharimu fedha nyingi ambazo zitailazimisha Serikali kukopa fedha nyingi, hali ambayo itaathiri deni la taifa ambalo kwa sasa Dola bilioni 26.
Nape ameongeza kwamba “Huu mpango wako mzuri lakini rudini kwenye mawazo ya kutumia sekta binafsi. Tukienda hivi tunaenda kuua uchumi,”.