Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa Marekani haitavumilia biashara yenye upendeleo, katika hotuba yake iliojaa malalamishi katika mkutano wa mataifa ya bara Asia na yale yaliopo katika bahari ya Pacific.

Amesema kuwa Marekani imejiandaa kushirikiana na mataifa ya Apec iwapo kutakuwa na bishara yenye kutopendelea upande wowote.

Bwana Trump alisema kuwa biashara huru iliathiri kazi za mamilioni wa raia wa Marekani na sasa anataka usawa kutekelezwa.

Tayari ameitembelea China na Japan katika zaira yake ya mataifa matano ya bara Asia.Apec unaleta pamoja uchumi wa mataifa 21 kutoka eneo la Pacific ambao ni asilimia 60 ya uchumi wote duniani.

Tangu achukue mamlaka rais Trump ameiondoa Marekani katika muungano wa Trans-Pacific, ambao unahusisha mkataba mkubwa wa kibishara unaoshirikisha mataifa 12 ya Apec akidai kwamba utaathiri uchumi wa Marekani.

Katika hotuba yake siku ya Ijumaa rais Trump alilishutumu shirika la biashara duniani WTO ambalo hutengeza sheria za biashara duniani na kusema haliweza kufanya kazi zake vyema iwapo wanachama wake hawataheshimu sheria hizo.

Alilalamika kuhusu ukosefu wa usawa wa kibiashara akisema Marekani imeondoa vikwazo vya kibishara huku mataifa mengine yakikataa kufanya hivyo.

Lakini hakuyalaumu mataifa ya Apec na badala yake kulalamikia watawala wa awali wa Marekani kwa kutoingilia swala hilo na kurekebisha hali.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *