Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) amekosoa mpango wa kujengwa kwa Uwanja wa Ndege wilayani Chato mkoani Geita.
Mbunge huyo amesema kuwa mpango ho hauna faida yoyote kwa Taifa kwani Rais Magufuli akishatoka madarakani hakuna ndege itakayokuwa inakwenda huko.
Mbilinyi amesema kwamba suala la kwamba wakikosoa kuhusu ujenzi wa uwanja wa ndege wa Chato ni kuchukulia kama suala binafsi bali ni suala la Mipango.
Pia amesema kuwa “Tukianza kuongea hivi kuna watuu wanawaka lakini mkumbuke hii siyo ‘personal’ bali nazungumzia ‘Principal’. Mnashindwa kwenda Butiama kwa Baba wa Taifa mtaenda Chato?
Pamoja na hayo Mbilinyi ameitaka serikali itumie mbinu ya waliyoitumia kwenye kukuza biashara ya Korosho itumie mbu hizo pia kwenye kukuza bei ya mazao mengine nchini kama mbaazi, Tumbaku na mazao mengineyo.
Hata hivyo Mbilinyi amewaasa mawaziri kutoshindana kutoa matamko ambayo wanajua hayawezi kutekelezeka bali watumie nafasi zao katika kumshauri Rais ili kusonga mbele kutekeleza mipango.