Mshambuliaji wa klabu ya Yanga, Obrey Chirwa amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)  kwa mwezi Oktoba.

Chirwa ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, beki Erasto Nyoni wa Simba na mshambuliaji Ibrahim Ajibu wa Yanga.

Mshambuliaji huyo alitoa mchango mkubwa kwa Yanga mwezi huo ikipata pointi saba katika michezo mitatu iliyocheza na kupanda katika msimamo wa ligi kutoka nafasi ya sita iliyokuwepo mwezi Septemba hadi ya pili mwishoni mwa Oktoba.

Yanga iliifunga Kagera Sugar mabao 2-1 Uwanja wa Kaitaba, Bukoba,  ambapo Chirwa alifunga bao moja na kutoa pasi ya mwisho ya bao moja.

Pia Yanga iliifunga Stand United mabao 4-0 Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, ambapo Chirwa alifunga bao moja na kutoa pasi ya mwisho ya bao moja.

Pia Chirwa alishinda gori kwenye mechi ya kati ya Yanga na Simba na kufanya matokeo kuwa 1-1 kwenye mechi iliyofanyika katika uwanja wa Uhuru jini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *