Muigizaji wa Bongo Movie, Chuchu Hans amesema kuwa iwapo akiachana na mpenzi wake Ray hatotaka tena mwanaume kutoka Tanzania.

Chuchu Hans amesema kuwa iwapo ataachana na mwenza wake huyo, hatakuwa kwenye mahusiano tena na mtu yeyote hususani wa hapa Tanzania.

Amesema kuwa “Kuachana kupo kwa sababu kila kitu Mungu ndio anapanga, kwa hiyo mimi siwezi kushindana na Mungu, kama ikitokea itakuwa imefikia mwisho wetu, sidhani kama nitakuwa tena na mwanaume tena hapa Tanzania, sidhani, yaani sijui kama nitaingia kwenye mahusiano, nitakaa muda mrefu bila mahusiano”.

Pamoja na hayo muigizaji huyo amekanusha tetesi za kuachana na mzazi mwenzake Ray Kigosi, baada ya kuwa na tetesi kuwa wawili hao wameachana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *