Waziri wa mambo ya nje nchini Kenya, Amina Mohamed ameilalamikia serikali ya Tanzania kufuatia hatua ya kuwapiga mnada zaidi ya ng’ombe 1,300 kutoka Kenya walioingia nchini humo kinyume na sheria.

Hatua hiyo inajiri siku moja tu baada ya Rais Magufuli kusema kuwa Tanzania sio shamba la mifugo wa taifa jirani.

Akizungumza katika mkoa wa Kagera ambako alikuwa katika ziara yake ya kikazi Rai Magufuli alisema kwamba Tanzania sio shamba la kuchungia mifugo ya nchi jirani na kwamba ataichukulia mifugo hiyo hatua kali za kisheria.

Vilevile alizitaka nchi Jirani kuchukua hatua kama hiyo iwapo mifugo ya Tanzania wataingia katika mataifa hayo kinyume na sheria.

Hatua ya kuwapiga mnada ng’ombe hao ilizua hisia kali miongoni mwa wafugaji wa Kenya baada ya wenzao waliokuwa na mifugo hao kukamatwa na kuzuiliwa kwa kuingia nchini humo kinyume na sheria.

Kufuatia hatua hiyo waziri wa mambo ya nje nchini Kenya Amina Mohammed alidaiwa kuanzisha mazungumzo kati ya serikali hizi mbili kutatua mzozo huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *