Wanafunzi sita wa shule ya msingi Kihinga wilayani Ngara mkoani Kagera wamfariki dunia na wengine zaidi ya 40 wamejeruhiwa baada ya kulipukiwa na bomu wakati wakicheza.

Kamanda wa polisi wa mkoa, Augustine Orom huo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na tayari wananchi wamejitokeza kuchangia damu kwa ajili ya kuwasaidia majeruhi.

Kwa mujibu wa Dokta Mariagoreth Fredrick ambaye ni mganga mkuu hosipitali ya Rurenge, amethibitisha kupokea miili hiyo na majeruhi ambao baadhi wako katika hali mbaya na tayari wanapatiwa matibabu.

Dokta huyo amesema kuwa wagonjwa walionao hapo hali zao si nzuri kutokana na kuvuja damu nyingi hivyo wananchi wameombwa kuchangia damu.

Pia Dokta Mariagoreth amesema  wanafunzi wengine wameumia matumbo, wengine wamechanika bandama, wengine wamevunjika miguu, wengine vichwa vimepata majeraha, wengine wameumia macho.

Inaelezwa kwamba kabla ya kulipukiwa na kifaa hicho kinachoarifiwa kuwa ni bomu, wanafunzi hao walikuwa wanakichezea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *