Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Lavalava amefunguka na kusema kuwa aliwahi kuishi nyumbani kwa mwanawake bila kujua kwamba mwanamke huyo amepangiwa nyumba hiyo na mwanaume mwingine.
Lavalava amesema baada ya kuishi pamoja alikuja kugundua nyumba wanayoishi na mwanamke huyo kapangiwa na mpenzi wake.
Amesema kuwa mwezi mmoja kabla hajaachia ‘Tuachane’ alikuwa na mpenzi wake ambaye walipanga mambo mengi ya maisha yao ya baadae na mwanamke alikubali ombi la mwanamuziki huyo.
Lavalava amesema kuwa kuna siku yupo ndani kwa mwanamke akaona jamaa anaingia ndani na kumwambia mimi ndiyo mwenye nyumba nimerudi hapa ni kwangu, Lavalava akasema kusikia hivyo alichanganyikwa sana.
Ameendelea kwa kueleza kuwa baada ya hilo kutokea waliongea na kujitetea kwa kutoa maelezo ambayo yatakuwa sawa kwa pande zote na kilichofuata ni kwenda kutoa ngoma ‘Tuachane’.