Mwanamuziki wa nyimbo za Injili nchini, Rose Muhando anatarajiwa kurudi tena kwenye game baada ya kukaa kimya zaidi ya miaka miwili.

Imepita muda wa takribani miaka miwili au zaidi tangu msanii huyo awe kimya katika muziki wa injili hapa nchini.

Aliyekuwa meneja wa msanii huyo Alex Msama amesema kuwa ni kweli rose muhando yupo kimya kwa muda mrefu lakini hiyo yote ilisababishwa na yeye mwenyewe kwa sababu kuna kipindi alikuwa ameendekeza tabia ya utapeli kwa mashabiki zake.

Msama amesema kuwa kulikuwa na kesi nyingi sana polisi zilikuwa zikimhusu, lakini kwa sasa anampngo wa kumrudisha tena kwa mashabiki ili aendelee kuwaburudisha mashabiki zake kwa sababu kwa sasa msanii huyo maebadilika kabisa na ana imani atafanya vizuri tena kama hapo awali.

Hii itakuwa ni moja ya habari njema kwa mashabiki wa injili kwa sababu nyimbo za Rose Muhando zilikuwa zikipendwa na kuchezwa na watu wa kila rika na kila dini kutokana na uzuri wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *