Klabu ya Azam FC wametangaza kuachana na mshambuliaji kutoka nchini Ghana, Yahaya Mohammed baada ya kushindwa kuonesha kiwango kizuri.
Azam FC wamefikia hatua hiyo baada ya kuona Yahaya Mohammed ameshindwa kuonyesha kile walichokitarajia.
Hayo yamesemwa a na msemaji wa klabu hiyo, Jaffary Idd baada ya kuzungumzo na mchezaji huyo kuhusu mkataba wake na klabu hiyo.
Maganga amesema tayari wameshampatia release letter na pamoja na hayo tayari wameshampatia kila kitu ikiwemo tiketi ya ndege ambapo wanatarajia ataondoka kurudi kwao Ghana Jumanne hii.
Mbadala wa Yahaya Mohamed kwa mujibu wa Afisa Habari Jaffary Maganga ni kwamba atatangazwa baada ya benchi la ufundi kufanya tasmini na kuchambua wale wanaowahitaji.
Mshambuliaji huyo alijiunga na Azam akitokea Aduana Stars ya Ghana, ambayo aliisaidia kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Ghana msimu 2015/16, Mohammed pia aliiibuka mfungaji bora namba mbili wa ligi hiyo kwa mabao 15 aliyofunga nyuma ya Latif Blessing wa Liberty Proffesional aliyetupia 17.
Mohammed alikuwemo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Ghana kilichoshiriki fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zilizofanyika mwaka juzi nchini Afrika Kusini na timu hiyo kuwa washindi wa pili.