Muigizaji wa Bongo Movie, Vicent Kigosi maarufu kama Ray amesema kuwa hawezi kumuonea wivu Dogo Janja baada ya kumuoa Irene Uwoya.

Kauli hiyo ya Ray imekuja baada ya baadhi ya watu kudai muigizaji huyo anaona wivu kutokana na ndoa hiyo kwasababu alikuwa mtu wake hapo awali.

Raya amesema kuwa yeye hawezi kufanya hivyo kwasababu alikuwa wa kwanza kumuona Irene Uwoya kabla ya Dogo Janja lakini hakuwaza kumuoa kwa hiyo hawezi kufanya hivyo kabisa.

Ray ameongeza kwa kusema kuwa alianza kumuona Irene kabla ya Dogo Janja, lakini hakuvutiwa kumuoa, hivyo hawezi kuwa na hisia za wivu kwa yeye kumuoa muigizaji huyo.

Ray ameendelea kusema kwamba yuko tayari kumuita Dogo Janja shemeji kwa sababu ameshamuoa dada yao Irene Uwoya, na kuhusu suala la umri halijalishi sana kwani kikubwa ni upendo.

Hivi karibuni Dogo Janja na Irene Uwoya wamefunga ndoa jambo ambalo limewashtua watu wengi, kwa kuwa kuna tofauti kubwa ya umri kati ya wawili hao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *