Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla amesema viongozi wote waliohusika na rushwa kwenye wizara hiyo watafikishwa kwenye mkono wa sheria.

Waziri ameyasema hayo alipotembelea hifadhi ya Serengeti katika pori tengefu la Loliondo ambapo amesema kuna kikundi ndani ya wizara kimekuwa kikiendesha vitendo vya rushwa kikihusisha wakurugenzi na mawaziri waliomtangulia.

Waziri Kigwangalla amesema kuwa anafahamu kuwa kuna ugawaji wa vitalu kinyume na sheria amesitisha na atafuatilia vitalu alivyogawa waziri Nyalandu kinyume na hatua itachukua mkondo wake.

Kigwangalla amesema kuwa atafukua mafaili yote na kuwaondoa mmoja baada ya mwingine na kuwafikisha kwenye mkono wa sheria wote waliohusika na vitendo hivyo ikiwemo kuwauza wanyama hai nje ya nchi.

Pia amesema kuwa hawezi kuendelea kufanya kazi mpaka asafishe uozo uliopo ndani ya wizara hiyo kwa maagizo ya rais.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *