Kiungo wa Simba, Said Ndemla ambaye amepata nafasi ya kufanya majaribio ya soka la kulipwa katika klabu ya AFC Eskilstuna nchini Sweden sasa anatarajiwa kusafiri Novemba 9 mwaka huu badala ya leo.

Kupitia taarifa ya klabu hiyo imesema kuwa safari ya kiungo imesogezwa mbele hadi ya siku ya Alhamisi.

 Taarifa hiyo imesema

Tunapenda kuwafahamisha kuwa safari ya mchezaji wetu Hamis Said Juma Ndemla iliyokuwa ifanyike leo Jumanne imesogezwa mbele.

Ndemla ambaye amepata nafasi ya kwenda kufanya majaribio katika klabu ya AFC Eskilstuna inayoshiriki ligi kuu nchini Sweden, sasa ataondoka nchini siku ya Alhamis ya tarehe 9 ya mwezi huu.

Mabadiliko haya ya safari hayataathiri muda wake wa majaribio katika klabu hiyo,ambapo atakuwa huko kwa siku 14.

Imetolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano,

Simba Sports Club.

Haji S.Manara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *