Mwanamuziki wa Marekani, Meek Mill amehukumiwa kwenda jela miaka miwili hadi minne kutokana na majaribio ya uhalifu aliyofanya.

Hukumu hiyo imetolewa jana ambapo rapper huyo alionekana mahakamani hapo kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo.

Hukumu hiyo imekuja baada ya kukamatwa kwa kosa la kupigana kwenye uwanja wa ndege wa St. Louis na kuendesha gari kwa fujo mjini New York City.

Baada ya hukumu hiyo Jay Z amelaani hukumu hiyo akidai kuwa imemuonea Meek Mill kutokana na kukiukwa kwa shiria.

Kwa upande wa mwanasheria wa mwanamuziki huyo amesema kuwa watakata rufaa kuhusu hukumu hiyo kwani imeshindwa kuzingatia sheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *