Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amesema kuwa endapo chama Cha Mapinduzi (CCM) hakitataka kuambiwa ukweli na kukosolewa utakuwa mwanzo wa kuanguka.

Nape aliyewahi kuwa katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho, amesema endapo CCM itaua utamaduni wa kukosoana kupitia vikao itapoteza mwelekeo.

Amesema hayo juzi nyumbani kwake eneo la Kisasa mjini Dodoma katika mazungumzo maalumu na Mwananchi.

Nape ambaye leo anatimiza miaka 40 ya kuzaliwa ameeleza kusikitishwa na namna ya baadhi ya watu aliowaita “vijana wa CCM”, kupotosha kwa makusudi kauli na ujumbe wake anaoutuma kupitia mitandao ya Twitter na Instagram.

Mbunge huyo alisema husikitika anaposoma namna kauli zake zinavyopotoshwa, huku wengine wakidai anatumia maneno makali kwa vile ameondolewa kwenye uwaziri alikokuwa waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Amesema akiwa katibu wa itikadi na uenezi kuna vikao vilifanyika mpaka saa sita usiku na alikuwa mkorofi kidogo kwa sababu maneno yake wakati mwingine yalikuwa magumu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *