Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Dudu Baya amesema kuwa wanawake wa Tanzania wana kawaida ya kulazimisha ndoa hasa wanapopata ujauzito hata kama ni kwa bahati mbaya.
Dudu Baya amesema kwamba jambo hilo haliingii akilini kwani walipokutana hawakukubaliana kuona.
Dudu Baya “Mimi mwanamke wangu ni bapa, wanawake wa kitanzania ukishampa mimba ndo kashalazimisha ndoa, suala la ndoa ni makubaliano na kama ukimuacha ndo anaenda kukupiga misumari”,.
Pia Dudu Baya amesema kwa sasa anatamani angeoa, kwani tayari ana watoto ambao wengine ni wakubwa.