Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Madee amefunguka na kusema kuwa anachukizwa na baadhi ya watu ambao wanadai ndoa ya Dogo Janja na Irene Uwoya ni kiki ya kazi zao.
Madee amesema kuwa kitu hicho ni kibaya sana kwani kuna uwezekano msanii akawa anahitaji msaada wa haraka na watu wakachukulia hilo kama kiki.
Madee amesema kuwa “Kitu ambacho nimekigundua na ni kibaya na kinaendelea kutokea ni watu kuamini katika kiki, hata leo ikitokea nimegongwa na gari nakuumia watu bado wataamini ni kiki na kushindwa kunisaidia,”.
Msanii huyo amesema kuwa suala lingekuwa la kumsaidia Dogo Janja ili aokoke kwenye jambo labda ni baya basi tungekuwa tumeshamuumiza kwa sababu watu wote wanaamini kwenye kiki.
Dogo Janja na Irene Uwoya walifunga ndoa yao October, 28 mwaka huu kwa mujibu taarifa za mitandao ya kijamii lakini September 4 ndipo Dogo Janja aliweka wazi hilo kuwa wamefunga ndoa.