Kiongozi wa Chama cha ACT – Wazalendo, Zitto Kabwe, leo ameripoti kituo cha Polisi Chang’ombe kama alivyotakiwa kufanya hivyo.

Baada ya kuripoti Polisi wamemueleza kuwa anapaswa kuripoti tena kituoni hapo Ijumaa ijayo, Novemba 17 mwaka huu.

Kwa uapande wake katibu wa Itikadi, Mwasiliano ya Umma na Uenezi wa chama hicho, Ado Shaibu ameeleza kuwa Kadhia hii inahusisha baadhi ya maneno katika hotuba yake ya Oktoba 29, 2017 alipokuwa kwenye mkutano wa kuzindua kampeni za udiwani katika Kata ya Kijichi, Wilayani Temeke.

Zitto aliongozana na timu ya mawakili wa chama pamoja na mke wake kituoni Chang’ombe.

Kwa sasa Kiongozi wa Chama wa chama hicho anaelekea kituo cha polisi Kamata, ambapo Mwenyekiti wa Chama, ndugu Yeremiah Maganja, pamoja na Katibu Mkuu, ndugu Dorothy Semu, wameitikia wito wa Kamishna wa Makosa ya Jinai (DCI) wa Jeshi la Polisi kituoni hapo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *