Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mimi Mars amesema kwa sasa anatamani Jux na Vanessa Mdee warudiane na waishi kama zamani.
Muimbaji huyo ambaye ni ndugu wa damu na Vanessa amesema kuwa anakuchukizwa na taarifa zinazodai kuwa anatoka kimapenzi na Jux baada ya kuachana na Vanessa.
Amesema kuwa “Kwanza nilikasirika kwa sababu ni kukoseana heshima, ina maanisha watu wananionaje kwanza, mnanichukuliaje kwamba mimi naweza nikafanya tendo na mtu wa dada yangu haileti maana kabisa, niliipuuzia ndio maana sijaizungumzia”.
Pia ameongeza kwa kusema kuwa “Mungu akijalia kweli I wish warudiane maana yake walikuwa poa, (Jux) ni mtu mcheshi, ana upendo, mtu mkarimu na ni mtu anayempenda Vanessa Mdee” .
Alipoulizwa anauchukuliaje ukaribu wa sasa kati ya Jux na Vanessa, alijibu; “kama mimi naona ni marafiki kama walivyotuambia ambao wanaendelea kuwa na uhusiano mzuri, maana tumejiwekea watu wakiachana lazima wawe maadui siyo lazima iwe hivyo, kwa hiyo wao wanatuonyesha njia tofauti”.