Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye amesema kuwa atashughulikia mapungufu akiwa ndani na siyo nje.

Kauli hiyo ya Nape imekuja baada ya Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu kujivua ubunge na kujiondoa katika chama cha Mapinduzi(CCM).

Nape kupitia ukurasa wake wa twitter ameweka picha inayomuonyesha mbunge huyo na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Ndg Kinana wakiwa wameweka kwa pamoja alama ya kidole gumba.

Ameanza kwa kuandika “Chama cha siasa ni ITIKADI, itikadi ni IMANI.Siamini SANA katika kubadili Imani KIENYEJI.Nitashughulikia MAPUNGUFU nikiwa ndani sio NJE”!

Nyalandu alikihama chama cha Mapinduzi Oktoba 30 mwaka huu ambapo alieleza kuwa amechoshwa na mwenendo wa siasa wa sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *