Kocha wa Simba, Joseph Omog ametamba kuvunja rekodi ambayo klabu hiyo inayo ya kutoshinda mechi mbili mfululizo katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Kocha Omog ameandaa mpango mkakati maalumu ambao utakiwezesha kikosi chake kuibuka na pointi sita kwenye mechi mbili wanazokwenda kucheza Nyanda za Juu Kusini.
Omog amesema kuwa amepania kuhakikisha timu yake inavunja rekodi ya Yanga kwa kushinda mechi hizo mbili ingawa amekiri kuwa siyo jambo dogo.
Omog amesema anaziheshimu timu za Mbeya City na Tanzania Prisons, lakini msimu huu ataomba wawasamehe kwani wamejipanga kuhakikisha wanarudisha heshima na hadhi ya Simba.
Timu ya Simba haijawahi kushinda mechi mbili mfululizo kwenye Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.