Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Ferouz amekanusha tuhuma zinazomkabili kuwa anatumia madawa ya kulevya.

Ferooz ni moja Kati ya wasanii wa kipindi kirefu ametuhumiwa kujihusisha na matumizi ya madawa ya Kulevya ambayo ndio yamepelekea kupotea katika ramani ya muziki.

Ferooz amezikana kwa nguvu shutuma hizo na kudai kuwa taarifa hizo hazifai kuaminiwa na watu wanaozisambaza ni wale wenye nia ya kumchafua na wasio mtakia mema.

Pia msanii huyo alielezea nia yake ya dhati ya kutaka kurudi kufanya muziki hivi karibuni kwa kutangaza kuwa anategemea kutoa ngoma yake hivi karibuni.

Wasanii wengi waliokuwa wanafanya vizuri siku za nyuma huishia kuchukua njia mbaya na hivyo kuishia kujiingiza katika matendo maovu kama kuuza na kutumia madawa ya kulevya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *