Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Barakah The Prince amedai kuwa YouTube account yake inafanyiwa mchezo mchafu ili ishusha idadi ya views.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Sometimes’ amesema kuwa views za ngoma yake hiyo zimekuwa zikishuka na kupanda na hata muda mwingine comment kufutwa.

Amesema kuwa kuna baadhi ya nchini ikiwemo China mashabiki wake wamekuwa wakilalamika haiwapati video yake lakini video za wa wasanii wengine zinapatikana.

Hata hivyo ameweka wazi kuwa watu wenye access ya kuendesha account yake hiyo ni Mx Carter na Seven Mosha wa RockStar4000 kutokana na makubaliano ya hapo awali, pia ameeleza kuwa yupo katika utaratibu wa kufuta account hiyo na kufungua nyingine.

Ngoma ya Barakah ‘Sometimes’ video yake ilitoka October 28 mwaka huu lakini hivi sasa haipatikani YouTube.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *