Mama mzazi wa msanii Dogo Janja amefunguka na kusema kuwa alikuwa na taarifa ya mwanae kuoa tangu mwaka jana.
Mama huyo amesema kuwa mara ya kwanza Dogo Janja hakumwambia kama anafunga ndoa na mwanamke gani.
Amesema kuwa hata baada ya kuambiwa kuwa Irene Uwoya ndio mwanamke anaeolewa na mwanae bado hakusita kutoa baraka kwa sababu anaamini kuwa huo ni uamuzi wake.
Hata hivyo mama huyo alipoulizwa kuhusu mwanamke aliemuoa mwanae,mama mzazi wa Dogo Janja alisema kuwa alikuwa anajua kabisa na kwa dini yao kuona ni suna.
Pia mama Dogo Janja amesema kuwa yeye na Irene Uwoya hawajawahi kuonana lakini wamekuwa wakiwasilina sana , na kuna kipindi Irene alikwenda Arusha lakini yeye hakuonanan nae, kuhusu mahusiano yake na mkwewe huyo mama anasema kuwa Irene amekuwa akituma zawadi mbalimbali kwa mama mkwe wake huyo na wanawasilina karibia kila siku.
Mama mzazi wa Dogo Janja amenasema kuwa ingawa ndoa imekuwa ya haraka haraka lakini wanategemea kufanya sherehe kubwa ya harusi itakayo fanyika Arusha kwa ajili ya familia kumtambua, na kwa upande wake yeye ameridhika kabisa wala hana wasiwasi na uamuzi aliochukua mwanae.
Ndoa ya Irene Uwoya na Dogo Janja ilifungwa wiki iliyopita na kuacha gumzo katika mitandao kutokana na umri wa watu hao wawili kupishana sana na hata hivyo wawili hao walishakataa sana kuhusu kuwepo kwa mahusiano baina yao.