Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Barakah The Prince amekanusha kumwagana na mpenzi wake ambaye ni mwanamuziki mwenzake, Naj baada ya kutoonekana wakiwa pamoja.
Baraka amesema hayo baada ya kuenea taarifa kuwa wawili hao wameachana kwasasa kutokana na kutoonekana pamoja na kutowekana katika mitandao ya kijamii kama hapo awali.
Barakah amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na Naj kwa kipindi kirefu sasa ambapo siku za nyuma walikuwa ni kawaida yao kuposti picha mtandaoni wakiwa pamoja au kila mmoja kumposti mwenziye lakini taratibu hiyo ikapotea na ndipo wengi walidhani kuwa watakuwa wamemwagana.
Pia mwanamuziki amesema kuwa hawezi kusapoti kazi ya Naj kwasababu wote ni wanamuziki kwa hiyo kila mmoja atasapoti kazi kwa hiyo kutofanya hivyo siyo sababu za wawili hao kuachana.
Barakah amesema kuwa kazi na mapenzi haviwezi kuingiliana hata siku moja alimsapoti kwa kazi yake ilipoishia ndo hapo hapo kwani ile ni page yake hawezi kuposti vitu vya Uwoya.