Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe baada ya kukamatwa na Polisi na kuachiwa ametakiwa kukamatwa tena kwa amri ya ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).
Zitto aliyeachiwa kwa dhamana na kukamatwa tena, amepelekwa kituo cha polisi cha Kamata kwa mahojiano zaidi kuhusu tuhuma za kutoa lugha za kichochezi.
Maneno hayo yaliyopelekea Zitto kushikiliwa na kuhojiwa ni pamoja na kusema: “Wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kufanya uchunguzi na kuwakamata watu waliompiga risasi Mbunge Tundu Lissu.
Wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kueleza chanzo cha miili ya watu wanaookotwa kwenye fukwe za bahari kama Coco Beach.
Hivyo kuichagua CCM ni sawa na kuwaunga mkono waliofanya vitendo vya kumshambulia Tundu Lissu na wanaoua watu wanaookotwa kwenye fukwe.