Stori ambazo zimeshika headline sana siku mbili hizi ni hii ya Uwoya kuolewa na Dogo Janja huku yakiwa yanasemwa mengi ikiwemo ni kuwa wawili hao hawajafunga ndoa bali ni kiki tu kutoa wimbo mpya.

Stori inazidi kupata mkanganyiko kwani Irene Uwoya anayedaiwa kuwa ni bibi harusi na kuolewa na mwanaume mwingine kiukweli ni mke wa ndoa halali kabisa ya kanisani ya mcheza mpira kutoka Rwanda anayejulikana kama Ndikumana.

Ndikumana na Uwoya walioana miaka michache iliyopita na kwapamoja wana mtoto mmoja wa kiume.

Baada ya sakata hili kutokea watu wengi wamekuwa wakijiuliza inakuaje kuwa Uwoya anaolewa wakati tayari mke wa mtu? Jana kupitia ukurasa wake wa Instagram Ndikumana alimjibu shabiki aliyemuuliza kama kweli mkewe Uwoya ameolewa na Dogo janja na Ndikumana alijibu;

Huyo Irene aolewe asiolewe mimi sina habari naye nina msimamo wangu na maisha yangu binafsi mda mrefu tu, kwani sins habari na mtu nadeka zangu kwa mpenzi wangu”.

Ndikumana aliweka ujumbe huo akaambatanisha na picha ikimuonesha akiwa amekumbatiana kimahaba kabisa na mpenzi wake kuonesha hajaumizwa na ndoa ya Irene.

Ukweli wa ndoa ya Uwoya na Dogo Janja lilizidi kuingia doa baada ya jana msanii Keisha kuweka picha ya Uwoya na Dogo Janja na kusema kuwa ile ni kiki kwa ajili ya kundi la Tip top connection ambapo inasemekana wanataka kurudi upya na ngoma mpya hivyo haikuwa Ndoa ya kweli.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *