Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo amezindua Kiwanda cha Victoria Moulders kilichopo eneo la Igogo jijini Mwanza.

Kiwanda hicho kinashughulika na utengenezaji wa vyombo vya plastiki na vifungashio vya mifuko.

Rais Magufuli amewapomgeza wamiliki wa Kiwanda hicho ambacho kimetengeneza ajira kwa vijana zaidi ya 500 huku kikiwa kichocheo kikubwa cha ukuaji uchumi jijini humo kuendana na mkatakati wa serikali ya Awamu ya tano ya kufufua na kukuza sekta ya viwanda nchini.

“Ni jukumu letu kama taifa kuamua kusahihisha makosa au tuendelee na makosa, Nyaza kulikuwa na viwanda kila mahali, baada ya mzee Masele kuondoka viwanda vikapotea. Mzee Masele ndiye mtu peke aliyenichangia shilingi elfu 10 kwenda kuchukua fomu ya ubunge.

“Kiwanda hiki kimewapa ajira zaidi ya vijana 500, kisingekuwepo pengine wangekuwa majambazi. Nikupongeze waziri kwa utendaji wako na kuhakikisha Tanzania ya Viwanda inawezekana,” .

Aidha Rais Magufuli amezichangia mifuko 200 ya saruji kwa shule mbili za Kata ya Igogo ambapo kila shule itapewa mifuko 100. Pesa kiasi cha Sh. Milioni 3 amezikabidhi kwa diwani wa kata hiyo na mbunge wake ili watekeleze adhima ya kununua saruji za ujenzi wa shule hizo.

Pia amechangia pesa kiasi cha Sh. Milioni 1 kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Igogo, ambazo amemkabidhi katibu wa CCM Kata.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *