Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Baraka The Prince amekanusha taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa amefulia baada ya kuondoka lebo ya RockStar4000.

Tangu msanii huyo kuondoka katika label ya RockStar4000 kumekuwa na taarifa zinazodai msanii huyo kuyumba kiuchumi hadi kupelekea kuuza gari kitu ambacho amekikanusha.

Baraka amesema kuwa “Sijawahi kufanya hivyo, kwanini niuze gari yangu sema hizi fununu, watu wanatengeneza mastori”

Barakah kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake ‘Sometime’ aliyoitoa chini ya lebo yake BANA ambayo inamilikiwa na yeye pamoja na mpenzi wake Naj.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *