Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Ambene Yessaya ‘AY’ amefunguka na kusema kuwa bifu kati ya Mwana FA na Lady Jaydee ilimpa wakati mgumu.

AY amesema kuwa alipata wakati mgumu kuona wasanii hao hawazungumzi wakati wote ni rafiki zake lakini aliamini siku moja wataufunga ukurasa wa uhasama huo.

Baada ya ugomvi wa wawili hao kumalizika, AY amesema kuwa hivi sasa anafurahi kuona wawili hao wamemaliza tofauti zao na wanazungumza kama kawaida.

 AY amesema kuwa “Mimi nilikuwa napata wakati mgumu sana, kwasababu hawa hawaongei alafu wote washkaji, lakini ikafika time (muda) wakawa wanauliziana. Nikajua sasa hivi watakuwa sawa,”.

Kabla ya kukwaruzana mwaka 2013, AY na FA waliwahi kufanya kazi pamoja mara kadhaa. Moja kati ya ngoma waliyofanya pamoja iliyoteka mitaa ni ‘Alikufa Kwa Ngoma’, ‘Hawajui’, ‘Msiache Kuongea’, ‘Wanaume Kama Mabinti’.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *