Dereva Lewis Hamilton amefanikiwa kushinda taji la nne la dunia katika michuano ya Mexico grand prix licha ya kumaliza akiwa nafasi ya tisa baada kugongana na Sebastian Vettel.
Mafanikio ya Hamilton yanamfanya kuwa dereva wa Uingereza kufanikiwa zaidi katika historia akiwa amevunja rekodi ya Jackie Stewart.
Anaungana na Vettel na mfaransa Alain Prost wenye vikombe vinne katika mashindano hayo ya maarufu ya maagari.
Aligongana na Vettel wakati walipokuwa wakijaribu kupishana katika kona katika mashindano hayo.