Muigizaji wa Bongo Movie, Rose Alphonce ‘Muna’ amesema kuwa, anapitia katika kipindi kigumu sana cha kumuuguza mtoto wake lakini muda huohuo kukosa usingizi kutokana na kesi inayoendelea ya mdogo wake wa hiari, Elizabeth Michael ‘Lulu’.

Muna ambaye tangu kesi ya Lulu imeanza kusikilizwa hakosi kuwa naye mahakamani alisema, amekuwa kwenye kipindi kigumu kwa kuwa takribani miezi miwili anamuuguza mtoto wake mguu wenye majeraha lakini pia hapati usingizi kwa ajili ya kesi ya Lulu.

 Muna amesema kuwa “Yaani najiona kabisa kama huu mwaka ni wangu, maana pale Muhimbili walishanizoea kabisa, nimekaa muda mrefu nikimuuguza mwanangu mguu lakini ukiachana na hilo nahangaika na upande wa pili ishu ya Lulu mpaka nachanganyikiwa,”.

Lulu anakabili na kesi ya mauaji bila kukusudia ya aliyekuwa mpenzi wake Steven Kanumba miaka mitando iliyopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *