Mwanamuziki  wa Bongo Movie, Nikki wa Pili amefunguka mambo atakayoyafanya kama akiwa Rais wa nchi.

Nikki wa pili ametaja baadhi ya mambo muhimu atakayoyafanya endapo atakuwa raisi.

Mwanamuziki huyo ambae alishawahi kusema kuwa anampango wa kuingia kwenye siasa anaendelea kuthibtisha nia yake hiyo kupitia maneno yake.Katika vitu alivyoviorodhesha ni pamoja na :

1.Kikao kikubwa cha serikali yangu itakuwa sio baraza la mawaziri bali  mkutano mkuu wa kijiji au mtaa(kitaa kitaongea)

2.Kipimo kikubwa cha maendeleo itakuwa ni kupanda au kushuka kwa maisha ya watu sio vipimo vya kukua kwa uchumi au makusanyo ya fedha.

3.Mfumo wa elimu utajikita katika kupima learning na sio ufeli au kufaulu

4.Vyama vyenye nguvu vitakavyokuwa vikifanya mikutano na kuhoji serikali sio vyama vya siasa  bali vyama vya wakulima, wafanyakazi ,walimu, machinga , bodaboda madaktari na kadhalika.

5.Serikali itakuwa mdau mkubwa  uchumi na mukewezaji  atakuwa ni mkulima,mfugaji, mchimbaji mdogo,wavuvi wadogo na wafanyabiashara wadogo.

6,Ardhi, maji ,elimu ,afya, havitakuwa bidhaa bali hifadhi za jamii

7.Maisha bila maadili hayana maana , kila mtoto ni lazima afundishwe kuwa na  maadili , uaminifu,heshima,ujamii,upendo, bidii, na kujiamini.

8,Mahusiano na mataifa ya afrika  hayatakuwa na neno wahamiaji haramu , mwafrika hawezi kuwa haramu maana Afrika ni nyumbani kwake.

Nikki anasema kuwa maswali ataulizwa kipindi cha kampeni kikifika lakini anampango wa kuwa mgombea binafsi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *