Wapigakura nchini Kenya wamejitokeza kupigia kura kumchagua rais baada ya uchaguzi wa awali uliompa ushindi Uhuru Kenyatta kubatilishwa na mahakama ya juu lakini upinzani umesusia uchaguzi mpya.

Wakenya wanapiga kura leo katika uchaguzi mpya wa rais ulioghubikwa na kususiwa kwa upinzani, ambako bila shaka kutampa ushindi Rais Uhuru Kenyatta, lakini akiwa na mamlaka iliyopungua kutokana na ushiriki mdogo na kasoro katika mchakato mzima, ambazo tayari majaji na tume ya uchaguzi wamekiri zina uwezakno wa kusababisha changamoto za kisheria.

Akiwahutubia wafuasi wake katikati mwa jiji la Nairobi, kiongozi wa upinzani Raila Odinga alisema hatoshiriki katika uchaguzi huo mpya kwa sababu ya kushindwa kuwabadilisha makamishna wa tume ya uchaguzi baada ya mahakama ya juu kufuta matokeo ya uchaguzi wa awali uliofanyika Agosti nane.

Muongo mmoja tangu watu 1,200 kuuawa katika uchaguzi mwingine uliobishaniwa, Wakenya wengi wamekuwa wakijiandaa na uwezekano wa kutokea vurugu nyingine. Odinga aliwasihi wafuasi wake kubakia nyumbani na kutokabiliana na polisi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *