Polisi Kikosi cha Kuzuia Ghasia wamefunga eneo lote la viwanja vya Uhuru Park jijini kabla ya mkutano ulioandaliwa na muungano wa National Super Alliance (NASA) kwa ajili ya kiongozi wake mkuu Raila Odinga kutoa tamko zito kuhusu mchaguzi wa marudio kesho.

Maofisa wa polisi wakiwa katika sare zao wamesambazwa muda mfupi baada ya uongozi wa Kaunti ya Jiji la Nairobi kumwandikia kamanda wa Japhet Koome akipinga uwanja huo kutumiwa na Nasa.

Gavana wa Nairobi Mike Sonko amemtaka kamanda Koome kuhakikisha eneo hilo linakuwa na usalama akihofia unaweza kutumika kwa “mkutano ambao haujaruhusiwa”.

“Nimefahamishwa kwamba viongozi wa National Super Alliance (Nasa) wanapanga kutumia viwanja vya Uhuru Park kwa mkutano wa kisiasa leo. Hata hivyo, rekodi za uongozi wa jiji zinaonyesha hawajafuata utaratibu wa kupata kibali kwa ajili ya mkutano huo,”.

Sonko amesema hakuna mkutano utakaoruhusiwa kwenye viwanja hivyo bila ya ridhaa ya mamlaka husika na kutoka serikalini.

Gavana huyo ameongeza kwamba polisi wahakikishe wanaweka ulinzi ili kuzuia upinzani. “Kwa mamlaka niliyonayo, tafadhari hakikisha mkutano batili haufanyiki bila ya ridhaa yetu na sheria,”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *