Jeshi la polisi Kanda maalum Dar es Salaam limemkamata meneja hoteli wa Peackock kwa kutoa ukumbi na kuruhusu watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja kufanyia mkutano, kitendo ambacho ni kinyume na sheria.
Kamanda Mambosasa ameyasema hayo leo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari, na kusema kwamba serikali hairuhuhusu kuwepo kwa vitendo hivyo, na mtu yeyote atakayehusika kuhamasisha atachukuliwa hatua za kisheria.
Sambamba na meneja hoteli huyo ambaye hakutajwa jina lake, Kamanda Mambosasa amesema watu wengine 12 wamekamtwa kufuatia tukio hilo, wakiwemo raia wa kigeni wa Afrika Kusini
Watu hao waliokamatwa ni pamoja na raia wawili wa Afrika Kusini, Mganda mmoja na Watanzania 9, na watafikishwa mbele ya sheria hivi karibuni.