Bunge la Afrika Kusini leo linaanzisha uchunguzi unaohusu madai ya ufisadi wa kiwango cha juu zaidi serikalini.

Wale waliopiga ramli kuhusu ufisadi huo na maafisa mashuhuri wanatarajiwa kuitwa kutoa ushahidi wao.

Muda huu huenda ukawa wa kukosa amani miongoni mwa watu wenye ushawishi nchini Afrika Kusini.

Mawaziri, watu matajiri, mtoto wa rais na mashahidi wengine wengi, wanatarajiwa kuitwa mbele ya wabunge wanaochunguza madai ya ufisadi mkubwa nchini humo.

Inadaiwa kuwa familia moja yenye nguvu ya Gupta, imekuwa na ushawishi wa viwango vya juu serikalini, ili kuweza kujishindia kandarasi za serikali.

Familia hiyo ya Gupta imekana madai hayo sawa na rafiki wao Rais wa nchini hiyo Jacob Zuma.

Katika kipindi hiki cha misukosuko ya siasa kuhusu ni nani atakaye mrithi Zuma, uchunguzi wa wiki hii huenda ukawa na athari za aina yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *