Idadi ya watu waliouawa kwenye mlipuko mkubwa wa bomu katika eneo lenye shughuli nyingi kwenye mji mkuu wa Somalia, Mogadishu siku ya Jumamosi, imefikia watu 300 hadi sasa.

Takriban watu wengine 300 walijeruhiwa kwa mujibu wa AFP, wakati lori lililokuwa limejazwa milipuko lilipolipuka karibu na lango la hoteli.

Ahmed Alli ambaye ni muuguzi anayefanya kazi kwenye hospitali moja amesema kuwa miili 160 haikuweza kutambuliwa na hivyo ilizikwa na serikali jana.

Hilo ndilo shambulizi baya zaidi kutokea nchini Somalia tangu kundi la al-Shabab lianzishe harakati zake mwaka 2007.

Rais Mohamed Abdullahi “Farmajo” Mohamed alilaumu kundi la al-Shabab kwa shambulizi hilo katili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *