Timu zinazoshiriki ligi kuu Tanzania bara zimekabidhiwa vifaa mbalimbali na mdhamini mkuu wa ligi hiyo Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, Vifaa hivyo vilivyokabidhiwa kwa timu zinazoshiriki ligi hiyo vina thamani ya shilingi milioni 514,208,400 /=.

Akikabidhi vifaa hivyo jana jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Nandi Mwiyombella amesema kwa mara nyingine tena katika kuhakikisha ligi ya soka nchini inaenda vizuri Vodacom inakabidhi vifaa mbalimbali vya ligi ambavyo ni jezi mbalimbali, viatu vya mazoezi na mechi, soksi, vilinda ugoko, nguo za mazoezi, nguo za kawaida na gloves.

Mwiyombella amesema Vodacom inaendelea kudhamini ligi kuu kwa sababu soka ni mchezo unaopendwa sana hapa nyumbani ukiwa na washabiki wengi hivyo inapenda kuona wananchi ambao baadhi yao ni wateja wake wanapata burudani ya mchezo waupendao pia siku zote inaamini kuwa michezo ni ajira kubwa duniani kote ikiendelezwa inaweza kubadilisha maisha ya watu wengi na taifa kunufaika kwa mapato makubwa ya kodi kutoka katika sekta hii.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura amezitaka klabu zinazoshiriki ligi hiyo kuheshimu chapa ya mdhamini wakati wote wa mechi za ligi.

Wambula aliongeza kuwa TFF isingependa kutumia kanuni na sheria kuadhibu klabu inayokwenda kinyume, bali kila klabu izingatie masharti ya mdhamini kama ambavyo anavyotimiza haki yake ya kuwapatia vifaa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *